Acts 7:39-42

39 a“Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena. 40 bWakamwambia Haruni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza, kwa maana mtu huyu Musa aliyetutoa nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ 41 cHuu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe. 42 dNdipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii: “ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka
kwa miaka arobaini kule jangwani,
ee nyumba ya Israeli?
Copyright information for SwhKC